WAKAZI WA SIYOI WAHIMIZWA KUWEKEZA ZAIDI KATIKA KILIMO.
Wakazi wa eneo la siyoi katika kaunti hii ya Pokot magharibi wametakiwa kutia juhudi katika shughuli zao za ukulima ili kuimarika zaidi kiuchumi.
Ni wito wake afisa mkuu katika wizara ya kilimo na ufugaji kaunti hii Isaiah Pendou ambaye amesema kuwa serikali ya kaunti imewekeza zaidi kwa wakulima ili kuafikia moja ya ajenda nne kuu za serikali ya kitaifa ya utoshelevu wa chakula.
Aidha Pendou amewahimiza wakulima kutouza bidhaa pamoja na mifugo ambayo wamepewa na serikali na badala yake kuvitumia ili kujiimarisha kiuchumi.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na mkurugenzi katika shirika la climate smart kaunti hii ya Pokot magharibi Philip Ting’aa ambaye aliongoza zoezi la kuwakabidhi wakulima hao kuku alfu 3,518 miongoni mwa vifaa vingine vya kilimo.