WAKAZI WA SALAMA ENDEBES WAPOKEZWA HATI MILIKI.


Zaidi ya wanachama mia tatu kutoka shamba la salama eneo bunge la Endebes kaunti ya Trans nzoia wamepata hati miliki ya ardhi kupitia kwa serikali kuu kwenye shamba la ekari mia sita thelathini na moja huku baadhi ya viongozi kutoka eneo hilo wakitoa wito kwa wanasiasa kutoingiza siasa kwenye swala hilo.
Akihutubia wakaazi hao eneo la salama endebes waziri wa ugatuzi Eugine Wamalwa alikabidhi hati miliki hizo kwa wakaazi waliojawa na furaha kutoka kwa serikali kuu huku akiomba wanasiasa kujitenga katika kuingiza siasa kwenye swala hilo.
Kwa upande wake mshirikishi wa bonde la ufa George natembeya akiwatahadharisha baadhi ya viongozi ambao wamekuwa wakiwataka wanachama kuchangia pesa kuhusiana na hati miliki hizo.