WAKAZI WA RIWO WALALAMIKIA HUDUMA DUNI KATIKA KITUO CHA AFYA CHA CHEPTARANO.

Na Benson Aswani
Wakazi wa eneo la Naktobar katika wadi ya Riwo kaunti hii ya Pokot magharibi wameitaka serikali ya kaunti hii kushughulikia hali ya kituo cha afya cha Cheptarano.
Wakazi hao wamesema kuwa kituo hicho cha afya kinakabiliwa na upungufu mkubwa wa dawa hali ambayo inawapelekea wakazi kupitia wakati mgumu kupata huduma za afya, huku wakidai kuwa ni aina moja pekee ya dawa zinazopatikana katika kituo hicho.
Wamesema kuwa kituo hicho cha afya kinashughulikia idadi kubwa ya watu eneo hilo hali ambayo inapelekea kuisha haraka, wakitaka kiwango cha dawa ambazo zinasambazwa katika kituo hicho kuongezwa.