WAKAZI WA RIWO WALALAMIKIA HALI MBOVU YA BARABARA.
Na Benson Aswani
Wakazi wa eneo la Riwo kaunti hii ya Pokot magharibi wamelalamikia hali mbovu ya barabara za eneo hilo wakatika wadau husika kuhakikisha kuwa hali hiyo inashughulikiwa haraka iwezekanavyo.
Wakiongozwa na Lemu Purokopoi wakazi hao wamesema kuwa shughuli za uchukuzi eneo hilo zimetatizika pakubwa wakikabiliwa na hali ngumu kutafuta huduma muhimu kutokana na ubovu wa barabara hizo huku pia wakidai eneo hilo limeachwa nyuma kimaendeleo.
Aidha wakazi hao wamelalamikia ukosefu wa umeme eneo hilo hali ambayo inaathiri huduma mbali mbali ikiwemo za afya, ambapo wanalazimika kutafuta huduma hizo maeneo mengine licha ya kuwepo kituo cha afya cha Adurkoit.