WAKAZI WA POKOT YA KATI WAPATA AFUENI KUFUATIA TATIZO LA MTANDAO.


Wakazi wa eneo la Masol katika kaunti hii ya Pokot magharibi wamenufaika pakubwa tangu kuzinduliwa mradi wa kusambaza mtandao wa universal Service fund.
Mkuu wa wilaya eneo la pokot ya kati Jeremiah koishtumo amesema kuwa mradi huo umesaidia kuimarisha usalama kwani umerahisisha pakubwa mawasiliano miongoni mwa vitengo vya usalama kutokana na visa vya uvamizi na wizi wa mifugo huku pia vijana wengi wakipata ajira na kuasi visa vya wizi wa mifugo.
Akizungumza na wanahabari baada ya kuzuru eneo hilo, afisa katika mamlaka ya mwasiliano nchini CA Paul Kiage amesema kuwa kata ndogo 14 katika kaunti hii ya Pokot magharibi zimenufaika na mradi huo katika awamu ya kwanza, huku tano zikitarajiwa kunufaika katika awamu ya pili.
Wakazi wa eneo hilo wakiongozwa na kiongozi wa mtandao wa vijana Petang’iro Longre Keris wamepongeza mradi huo ambao wamesema umeimarisha hali yao ya maisha ikiwa kurahisisha huduma kwa wanaohitaji huduma za afya.