WAKAZI WA POKOT MAGHARIBI WATAKIWA KUWA MAKINI KATIKA UCHAGUZI MKUU UJAO.


Wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi wametakiwa kuwa makini katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao na kuwachagua viongozi ambao watawahudumia vyema pamoja na kutumia pesa za umma kwa uwazi.
Ni wito wake seneta wa kaunti hii Samwel Poghisio ambaye amedai kuwa wengi wa viongozi kaunti hii hasa wabunge wamekuwa wakitumia vibaya fedha ambazo zinatengewa miradi ya maendeleo maeneo bunge akisema viongozi kama hao hawafai kurejea tena uongozini.
Wakati uo huo Poghisio amerejelea hatua ya kubanduliwa spika wa bunge la kaunti hii ya Pokot magharibi Catherine Mukenyang akikariri kauli yake kuwa hatua hiyo ilichochewa na baadhi ya viongozi wakuu katika serikali ya kaunti hii.
Aidha amewahikikishia waliokuwa madiwani kuwa swala la kulipwa marupuru lipo bungeni na kuwa watapewa fedha hizo kutokana na majukumu makubwa waliyofanya katika utawala wa serikali zilizotangulia.