WAKAZI WA POKOT MAGHARIBI WATAKIWA KUKUMBATIA MTAALA WA CBC.


Wadau wa elimu katika kaunti hii ya Pokot magharibi wameendelea kuwahimiza wananchi kukumbatia mtaala mpya wa elimu CBC ambao wameutaja kuwa na manufaa makubwa kwani unaangazia maswala mengi na yenye manufaa kwa mwanafunzi ikilinganishwa na ule wa 8.4.4.
Wakiongozwa na afisa wa elimu eneo la Riwo eneo bunge la Kapenguria kaunti hii Daniel Loripo wadau hao wamewataka wazazi kutafakari kuhusu umuhimu wa mtaala huo na kupuuza madai ambayo yanaenezwa nchini kuuhusu na badala yake kutoa nafasi kwa serikali kuufanikisha.
Kauli yake inafuatia shinikizo ambazo zimeendelea kutolewa kwa serikali kusitisha utekelezwaji wa mtaala huo wengi wa wakazi kaunti hii wakisema kuwa serikali haijajiandaa vyema kutekeleza mtaala huo kwani walimu wengi hawajapata mafunzo ya kutosha kuufanikisha.