WAKAZI WA POKOT MAGHARIBI WATAKIWA KUKUMBATIA MBINU ZA UPANGAJI UZAZI.


Wito umetolewa kwa wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi kukumbatia mbinu za upangaji uzazi na kujitenga na dhana zinazoambatana swala la upangaji uzazi katika jamii.
Wataalam wa upangaji uzazi wakiongozwa na Peris Chepeng’at Wamesema kuwa upangaji uzazi una manufaa makubwa ikiwemo kuimarisha afya ya akina mama.
Aidha wamesema kuwa swala la upangaji uzazi si la wàtu wazima pekee bali pia linafaa kukumbatiwa na vijana waliofika umri wa kupata watoto.
Wakati uo huo wametoa wito kwa wazazi kujitenga na imani zilizopitwa na wakati na badala yake kuchukua jukumu la kuzungumza na wanao kuhusu swala la upangaji uzazi ili kukuza kizazi chenye maadili.