WAKAZI WA POKOT MAGHARIBI WATAKIWA KUJITOKEZA ILI KUFAHAMU HALI YAO YA HIV
Takriban watu alfu 4,312 wanaugua virusi vya hiv katika kaunti hii ya Pokot magharibi.
Haya ni kwa mujibu wa afisa anayesimamia mpango wa hiv katika kaunti hii Nelly Achokor ambaye hata hivyo amesema ni watu alfu 3,200 pekee ambao wanatumia dawa za kukabili makali ya virusi hivyo akiwataka wanaougua hiv kujitokeza ili kupokea dawa.
Kwa upande wake afisa anayetoa huduma ya kuwalinda kina mama walio na virusi hivyo dhidi ya kuwaambukiza wanao Penina Pulol ametoa wito kwa kina mama wajawazito kufanya mazoea kufika vituo vya afya ili kufahamu hali zao na kuhakikisha mtoto anasalia salama.
Ni wito ambao umesisitizwa na msimamizi wa shirika la ampath kaunti hii ya Pokot magharibi John Baraza ambaye pia amewataka wakazi kujitokeza ili kufahamu hali yao kuhusu virusi vya hiv akisema vipimo na dawa za hiv hutolewa bure katika vituo vyote vya afya .