WAKAZI WA POKOT MAGHARIBI WALALAMIKIA MAKADIRIO YA BAJETI.


Hisia mbali mbali zimeendelea kuibuliwa nchini kufuatia siku moja baada ya waziri wa fedha ukur yattani kusoma makidirio ya bajeti ya mwaka 2021/2022.
Wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi hasa wahudumu wa boda boda wamelalalamikia kupanda bei ya pikipiki na vifaa vya sekta hiyo wakisema huenda hali hii ikafanya wengi wao kujitenga na sekta hiyo na kuanza kujihusisha na uhalifu.
Wamesema kuwa makadirio hayo ya bajeti hayamfaidi kwa vyovyote mwananchi wa kawaida ila
kumkandamiza hata zaidi na kufanya maisha kuwa magumu zaidi nchini kenya kwa mkenya wa hali ya chini.