WAKAZI WA POKOT MAGHARIBI WAHIMIZWA KUTOHADAIWA NA MFUMO WA BOTTOM UP.
Kamishina wa kaunti hii ya Pokot magharibi Apolo Okelo amepuuzilia mbali mfumo wa kiuchumi wa naibu rais Willia Ruto wa Bottom up economic model.
Apolo amewataka wananchi kutohadaiwa na baadhi ya viongozi wanaojipigia debe kwa kutumia mfumo huo akisema kuwa hamna lolote geni kuhusiana na mfumo huo kwani umekuwepo tangu awali akisema serikali imekuwa ikiwahusisha pakubwa wananchi hasa maeneo ya mashinani katika miradi mbali mbali.
Wakati uo huo Apolo amewataka wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi kumakinika katika kuhusika kwenye utekelezwaji wa miradi ya maendeleo maeneo ya mashinani ili kuhakikisha miradi yote inayopasa kutekelezwa inatekelezwa kikamilifu.
Kwa upande wake katibu katika wizara ya maeneo kame Micah Powon amesema kuwa uhusiano kati ya serikali kuu na zile za kaunti umeimarika zaidi hasa katika muhula wa pili wa ugatuzi hali ambayo imepelekea kuimarika utoaji huduma.