WAKAZI WA POKOT MAGHARIBI WAENDELEA KUNUFAIKA NA MIRADI CHINI YA NRT.


Shirika la NRT Northern Rangelands Trust pamoja na mashirika mengine ikiwemo lile la E. For impact kwa ushirikiano na serikali ya kaunti hii ya Pokot magharibi limeendeleza miradi ya kuwanufaisha wakazi wa maeneo mbali mbali ya kaunti hii.
Akizungumza baada ya kuongoza zoezi la kutoa chanjo kwa mbuzi eneo la Turkwel mkurugenzi wa mipango katika shirika hilo Rebecca Chebet amesema lengo kuu la miradi inayotekelezwa na mashirika hayo ni kuhakikisha mkulima kaunti hii ananufaika kiuchumi.
Kwa upande wake mwakilishi wa umoja wa ulaya EU katika miradi hii Titus Katembu amesema kuwa miradi kama hii ya kuimarisha shughuli za ufugaji ambao ndio chanzo cha uchumi wa wakazi wengi wa kaunti hii itasaidia pakubwa kuimarisha uchumi wa kaunti hii.
Waziri wa kilimo kaunti hii Geofrey Lipale amepongeza ushirikiano kati ya mashirika hayo na serikali ya kaunti akisema umewafaa zaidi wakulima kwani wengi wa wakulima kaunti hii hupoteza asilimia 30 ya mbuzi kila mwaka kupitia magonjwa.