WAKAZI WA MUINO WALALAMIKIA HALI MBOVU YA MIUNDO MBINU.

Wakazi wa eneo la Muino katika kaunti hii ya Pokot magharibi wamelalamikia hali mbovu ya miundo mbinu eneo hilo.
Wakiongozwa na Abraham Toiyareng, wakazi hao wamesema kuwa bararabara za eneo hilo hasa ya kutoka chepara hadi Endough iko katika hali mbovu hali ambayo imeathiri pakubwa shughuli zao za kila siku ikiwemoi uchukuzi na kibiashara.
Aidha wakazi hao wamelalamikia kituo cha afya ambacho wamesema licha ya kuchukua muda mrefu kukamilika katika ujenzi sasa hakina dawa za kutosha hali inayowalazimu wakazi kusafiri mwendo mrefu kutafuta matibabu.
Wamesuta utawala wa gavana Lonyangapuo wakidai kuwa haujawafaidi ikilinganishwa na mtangulizi wake Simon Kachapin licha ya kuwa katika utawala wake hakuwa na mgao wa kutosha ikilinganishwa na sasa.