WAKAZI WA MASOL WALALAMIKIA UHABA WA MAJI NA MKALI YA NJAA.


Wakazi wa eneo la masol katika kaunti hii ya Pokot magharibi wamelalamikia uhaba mkubwa wa maji eneo hilo wakiomba serikali kuingilia kati kushughulikia hali hiyo.
Wakazi hao wamesema kuwa wanalazimika kutembea mwendo mrefu kutafuta raslimali hiyo muhimu ambapo hata hivyo ni kisima kimoja pekee ambacho wanalazimika kukitegemea.
Aidha wamelalamikia kukithiri makali ya njaa pamoja na uhaba wa lishe ya mifugo yao kukotakana na athari za ukame inaoshuhudiwa eneo hili, hali wanayosema imeathiri hata bei ya mifugo sokoni.