WAKAZI WA LOKIRIMO POKOT MAGHARIBI WATAKA KUPEWA MBINU ZA KUJIKIMU KIMAISHA.

Na Benson Aswani
Wakazi wa Lokirimo eneo la Kongelai kaunti hii ya Pokot magharibi wametoa wito kwa viongozi kuwatafutia mbinu za kutafuta riziki hasa baada ya kupigwa marufuku ugemaji wa pombe.
Wakazi hao wengi wao wakiwa akina mama wamesema kuwa walikuwa wakitegemea ugemaji pombe kama kipato chao cha kila siku na sasa wanakabiliwa na hali ngumu ya kukimu mahitaji yao baada ya biashara hiyo kupigwa marufuku.
Wakati uo huo wakazi hao wamelalamikia kufungwa vyoo eneo hilo hali inayowalazimu kutumia msitu ulio eneo hilo kwenda haja wakihofia usalama wao ikizingatiwa mtu mmoja aliuliwa katika msitu huo juma jana.
Wametaka viongozi kuingilia kati ili kuhakikisha vyoo hivyo vinafunguliwa.