WAKAZI WA KAPCHOK WAKADIRIA HASARA BAADA YA KUFA ZAIDI YA NG’OMBE 80
Zaidi ya familia 13 za wafugaji katika wadi ya kapchok kaunti hii ya Pokot magharibi wanakadiria hasara baada ya zaidi ya ng’ombe 80 kufa bila kujulikana kilichosababisha hali hiyo.
Mwakilishi wadi ya kapchok Peter Lokor amesema kuwa madaktari wa mifugo tayari wamefika katika eneo la tukio na kuchukua sampuli za damu na kinyesi ili kubaini ugonjwa ambao umepelekea hasara hiyo.
Hata hivyo wakazi hao wamesema huenda ugonjwa huo umesababishwa na mimea fulani yenye sumu ambayo imechipuka baada ya kushuhudiwa mvua kubwa.
Lokor amewasihi wakazi wa kapchok kuwalisha mifugo wao mbali na mito ambako inakisiwa mimea hiyo imeota.