WAKAZI WA KACHELIBA WALALAMIKIA UKOSEFU WA UMEME
Wakazi wa soko la Kacheliba kaunti ya Pokot magharibi wanalalamikia ukosefu wa nguvu za umeme wakisema wamekuwa kwenye giza kwa takriban wiki tatu sasa.
Wakazi hao sasa wanaitaka wizara ya kawi kuingilia kati ili kuwanusuru kwani huduma nyingi muhimu zimekosa kutekelezwa kutokana na ukosefu wa nguvu za umeme.
Aidha wameelezea hofu ya kuzuka visa vya ukosefu wa usalama ambao huenda ukashuhudiwa eneo hilo kutokana na hali hiyo.
Mbali na suala la umeme, wakazi hao wanalalamikia hali ya uchumi hasa kuongezeka kwa bei ya bidhaa nyingi hali wanayodai imesababishwa na hulka ya serikali kukopa madeni mengi