WAKAZI WA KABUCHAI WATAKIWA KUTUNZA MIRADI.

Na Benson Aswani
Wito umetolewa kwa wakazi wa Mukuyuni eneo bunge la Kabuchai kaunti ya Bungoma kutunza vyema miradi ya serikali ambayo inafadhiliwa kupitia ushuru wao ili kuondolea serikali gharama ya kuikarabati kila mara.
Akiwahutubia wakazi katika soko la Lukhome baada ya kuwakabidhi mitungi ya maji, kaimu kamishina wa eneo hilo July Mutura ambaye amesema kuwa serikali imekuwa ikitumia raslimali nyingi kukarabati na hata kujenga upya baadhi ya miradi anayosema kuwa inafaa kulindwa na wananchi.
Mwakilishi wadi wa eneo hilo Meshack Museveni amepongeza msaada huo akisema kuwa utasaidia pakubwa kutatua tatizo la maji safi ya kunywa kwa wakazi wa eneo hilo.
Aidha ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wakazi hasa vijana kutokubali kutumika na viongozi wa kisiasa kuzua vurugu katika mikutano na hafla mbali mbali kwa manufaa yao ya binafsi.