WAKAZI WA EWAN WALALAMIKIA BARABARA MBOVU POKOT KUSINI.


Wakazi wa eneo la Ewan eneo bunge la Pokot kusini kaunti hii ya Pokot magharibi wamelalamikia hali mbovu ya barabara eneo hilo wanayosema kuwa imeathiri shughuli nyingi muhimu.
Wakiongozwa na Mathew Chemer wakazi hao wamesema kuwa shughuli za usafiri zimeathirika huku wakilazimika kutumia fedha nyingi kusafiri kutafuta huduma mbali mbali ikiwemo za afya na kibiashara kutokana na hali mbaya ya barabara hiyo.
Wametoa wito kwa wadau husika kuchukua hatua za kuhakikisha barabara za eneo hilo zinashughulikiwa haraka iwezekenavyo.
Wakati uo huo wakazi hao wametaka serikali ya kaunti hii ya Pokot magharibi pamoja na wahisani kushughulikia uhaba wa dawa katika vituo vya afya eneo hilo pamoja na kuhakikisha wahudumu wa afya wa kutosha katika vituo hivyo ili kuimarisha huduma za afya kwa wenyeji.