WAKAZI WA ELGEYOI MARAKWET WATAKIWA KUDUMISHA AMANI WANAPOTARAJIWA KUELEKEA DEBENI.


Siku moja kabla ya kufanyika uchaguzi mdogo wa useneta kwenye kaunti ya elgeyo marakwet na kwingineko nchini wito unatolewa kwa Wakaazi wa eneo hilo pamoja na viongozi katika maeneo ambako utaandaliwa uchaguzi mdogo wadumishe amani wakati wa uchaguzi na hata baada ya uchaguzi wakisubiri matokeo
Kiongozi wa walio wengi kwenye bunge la kaunti ya elgeyo marakwet ambaye ni mwakilishi wadi ya kapchemutwa Stephen cheriot amesema japo kuna ushindani mkali baina ya wagombeaji wa useneta hakujashuhudiwa malumbano hadi sasa akisema hiyo ni dalili nzuri.
“Nawapongeza wananchi wote wa kaunti hii ya Elgeyo marakwet na wagombea wa useneta kwa kuendesha kampeni zao kwa njia ya amani na kuhakikisha kwamba hakuna mikwaruzano miongoni mwao ambayo ingepelekea migawanyiko miongoni mwa wananchi.” Alisema Cheriot.
Kinyanganyiro hicho cha seneta kina wagombea sita wakiwemo wiliam kipkemoi kisang wa chama cha UDA Pauline cherotich sei wa chama cha safina Timothy Tanui anayewania kwa chama cha new democrats huku Andrew Mengich na Kelvin Kemboi wakiwa wagombea huru.
“Kwa hizi kampeni za uchaguzi mdogo wa useneta kila mtu aliendesha kampeni zake kwa njia sawa na zimetamatika vyema. Nawaomba wakazi wa Elgeyo marakwet kuendelea kudumisha amani wakati wa watakapofika debeni na hata baada ya uchaguzi huo mdogo.” Alisema mmoja wa wakazi.
Kiti hicho cha useneta kilisalia wazi baada ya aliyekuwa seneta wa kaunti hiyo Kipchumba Murkomen kuteuliwa na rais William Ruto katika wizara ya barabara.