WAKAZI WA BUNGOMA WATAKIWA KUUNGA MKONO UDA.


Mbunge wa sirisia katika kaunti ya Bungoma John Waluke ametoa wito kwa viongozi na wananchi katika kaunti hiyo kujiunga na chama cha UDA kinachohusishwa na naibu rais William Ruto.
Akizungumza katika hafla moja ya mazishi eneo bunge lake la sirisia, waluke amedai kuwa mwananchi wa kawaida atanufaika pakubwa iwapo atamuunga mkono naibu wa rais William Ruto kuingia ikulu katika uchaguzi mkuu ujao hasa ikizingatiwa sera yake ya kuinua uchumi kutoka ngazi ya chini.
Wakati uo huo Waluke ameelezea kusikitishwa na ongezeko la utovu wa usalama katika kaunti ya Bungoma akiwataka wakazi wa kaunti hiyo kushirikiana kikamilifu na idara za usalama kwa kuwatambua watu wanaohusika na maswala ya utovu wa usalama katika kaunti hiyo.