WAKAZI WA BONDE LA KERIO WALALAMIKIA BAA LA NJAA.


Wakaazi wa maeneo ya bonde la kerio sasa wanaiomba serikali na mashirika mengine kuwasambazia chakula cha msaada ili kuwanusuru na baa la njaa linalowakumba.
Wakiongozwa na Timothy Kemboi wakazi hao wanasema kwamba watu wengi wamekuwa wakiishi kwa hofu hiyo hivo kushindwa kuendeleza shughuli za kuzalisha chakula kutokana na ukosefu wa usalama kwenye eneo hilo .
Aidha wengi wao wamelazimika kuhama makaazi yao na kutorokea maeneo ya usalama huku wakihitaji chakula cha msaada walikohamia.
Kwa mara nyingine, wakaazi hao wametoa wito kwa rais uhuru Kenyatta kuingilia kati swala la ukosefu wa usalama kwenye eneo hilo wakidai kwamba wakuu wa idara za usalama wameshindwa kurejesha amani.