WAKAZI WA BARINGO WALALAMIKIA UKOSEFU WA MAAFISA WA USAJILI KATIKA BAADHI YA VITUO VYA USAJILI.


Ikiwa imesalia takriban siku saba kabla ya shughuli ya usajili wa wapiga kura wapya kutamatika, baadhi ya wakazi katika kaunti ya baringo wamejitokeza na kulalamikia kutokuwapo maafisa wa usajili kwenye baadhi ya vituo vya upigaji kura.
Akizungumza katika eneo la pemwai mmoja wa wazee wa mtaa kwa jina william chebii rumuruti amewataka maafisa hao kufika katika maeneo yote ya kupigia kura ili kuwasajili vijana wanaolenga kuwa wapiga kura.
Rumuruti ameongeza kuwa gharama ya usafiri kwa baadhi ya wakazi imewazuia kufika katika kituo cha huduma kujisajili hivyo kuwataka maafisa hao kuwajibikia majukumu yao.
Aidha rumuruti amewashauri wakazi kujiepusha na viongozi wanaoeneza siasa za chuki na zinazoweza kuleta migawanyiko miongoni mwao huku pia akiwahimiza viongozi kuendesha siasa za amani.