WAKAZI TRANS WATAKIWA KUWA MAKINI KATIKA UCHAGUZI MKUU UJAO.

NA BENSON ASWANI
Wito umetolewa kwa wapiga kura Kaunti ya Trans Nzoia kumakinika zaidi mwaka huu kwa kuwachagua viongozi watakaohakikisha usimamizi bora wa rasilimalii zao mbali na utekelezwaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi.
Kwenye mkao na wanahabari mjini Kitale mwenyekiti wa wafanyakazi Kaunti ya Trans Nzoia Samuel Juma Kiboi amesema kwa miaka kumi sasa Kaunti ya Trans Nzoia imesalia nyuma kimaendeleo kwa kukosa uongozi bora unaohusisha wafanyakazi na umma akisema mwaka huu ni sharti umma kuchagua gavana na waakilishi wadi wachapakazi.
Wakati huo huo Kiboi amelaumu utendakazi duni wa serikali ya sasa wa miaka 10 kutokana na ukosefu wa uwazi na uwajibikaji kwa umma, akitaka watakao chaguliwa kuhakiiksha wanahusisha umma na washikadau wengine katika maamuzi muhimu ya utekelezaji wa maendeleo katika Kaunti.