WAKAZI TRANS NZOIA WATAKIWA KUENEDELEA KUJITOKEZA KUSAJILIWA KUWA WAPIGA KURA.

Na Benson Aswani
Viongozi katika kaunti ya Trans nzoia sasa wanawataka wakazi wa kaunti hiyo ambao walikosa kusajiliwa kuwa wapiga kura katika zoezi la usajili wa wapiga kura wapya ambalo limekuwa likiendelezwa na tume ya uchaguzi IEBC kufika katika afisi za tume hiyo ili kusajiliwa.
Mbunge wa saboti Caleb Hamisi amesema eneo bunge hilo lilitamazamiwa kusajili wapiga kura alfu 17,636 kufikia sasa lakini wameweza kusajili wapiga kura 7,383 pekee, akiwataka walimu kuwapa fursa wanafunzi waliotimu umri wa kuwa na vitambulisho kutafuta stakabadhi hizo na kujisajili kuwa wapiga kura hata wakiwa shuleni.
Ni matamshi yaliyoungwa mkono na kamishana wa Kaunti ya Trans-Nzoia Sam Ojwang akisema hadi kufikia sasa Kaunti ya Trans Nzoia imewasajili wapiga kura 28,702 hii ikiwa ni asilimia 36.7 ya waliosajiliwa, kinyume na watua alfu 78,026 waliotarajiwa, akitoa wito kwa asilimia 63.3 iliyosalia kutembelea afisi za IEBC maeneo bunge yao ili kusajiliwa.