WAKAZI TRANS NZOIA WAHIMIZWA KUWANGAZIA SERA ZA WANASIASA WALA SI VYAMA.


Ikiwa imesalia takriban miezi sita kabla ya uchaguzi mkuu wa terehe 9 mwezi agosti, wakazi katika kaunti ya Trans nzoia wameshauriwa kuangazia sera za wawaniaji wa nyadhifa za uongozi na wala sio vyama vyao vya kisiasa wakati wa kufanya maamuzi yao.
Akiongea baada ya kuhudhuria ibada ya jumapili katika kanisa la Kesogon P.A.G katika eneo la kapchorwa, mwaniaji huru wa wadhifa wa ugavana kwenye kaunti ya Trans nzoia Jim Nduruchi Wakhungu amewahimiza wakazi kuwachagua viongozi wenye sera na walio na rekodi ya utendaji kazi.
Wakhungu aidha amewasuta baadhi ya viongozi anaodai wanayatumia makundi ya vijana kuzua vurugu katika hafla za mazishi akisema kwamba ni kama dharau kwa familia iliyofiwa na mpendwa wao.
Wakati uo huo amewahimiza wanasiasa kujiepusha na matamshi ya chuki na yanayoweza kuibua uhasama baina ya wakenya wanapoendeleza harakati zao za kutafuta uungwaji mkono wa wananchi.