WAKAZI POKOT YA KATI WALALAMIKIA UHABA WA MAJI


Wakazi wa eneo la masol eneo la Pokot ya kati katika kaunti hii ya Pokot magharibi wamelalamikia uhaba wa maji ambapo wanalazimika kutumia bwawa moja la maji pamoja na mifugo yao na wanayama wa porini.
Wakazi hao wamesema kuwa uhaba wa bidhaa hiyo muhimu unawalazimu kung’ang’ania bwawa moja ambalo linapatikana eneo la Kotulupogh kila kuchao hali ambayo imesababishwa na kiangazi ambacho kimeshuhudiwa eneo hilo kwa kipindi kirefu.
Maeneo ambayo yameathiriwa zaidi ni pamoja na Chepkonoh, Kakauni, Kotulupogh, Lorach na
Tapareng.
wakazi hao wanasema kuwa kina mama wanalazimika kutembea zaidi ya kilomita 50 kila siku kutafuta maji wengi wao wakidaiwa kuathirika pakubwa kwa kutumia maji chafu huku wakitoa wito kwa serikali ya kuu nan ile ya kaunti kuchimba visima zaidi eneo hilo ili kuwanusuru.
Aidha wakazi hao wameelezea wasiwasi wa kuathirika na virusi vya corona kutokana na hali kuwa ni wakazi wengi wanaokutanika eneo hilo kuteka maji hali hamna kanuni zozote za kukabili maambukizi hayo zinazozingatiwa.