WAKAZI POKOT MAGHARIBI WATAKIWA KUWA MAKINI MSIMU HUU WA KRISMASI.


Wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi wametakiwa kuwa makini zaidi barabarani wakati wanaposafiri kuungana na jamaa zao msimu huu pamoja na kuhakikisha kuwa wanadumisha amani.
Akiwatakia wakazi wa kaunti hii heri njema ya krismasi na mwaka mpya, seneta Samwel Poghisio aidha amewataka madereva kuwa makini na kuzingatia sheria za barabarani ili kuhakikisha visa vya ajali za barabarani haviripotiwi msimu huu.
Aidha Poghisio amewataka wakazi kuzingatia kanuni za wizara ya afya ili kukabili maambukizi ya virusi vya corona na hasa kwa wale ambao hawajapokea chanjo dhidi ya covid 19 kuhakikisha wanapokea chanjo hiyo ikizingatiwa hali kuwa aina mpya ya virusi vya corona ya omicron ainaenea kwa kasi.
Wakati uo huo, seneta Poghisio ametoa wito kwa wazazi kuwa waangalifu katika matumizi ya fedha msimu huu na kuhakikisha kuwa wanahifadhi karo ya wanao mwaka ujao ikizingatiwa wanafunzi wanafunga shule kwa muda mfupi kufuatia mabadiliko katika kalenda ya masomo.