WAKAZI POKOT MAGHARIBI WATAKIWA KUWA MAKINI KATIKA UCHAGUZI MKUU UJAO.

Na Benson Aswani


Wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi wametakiwa kuwa makini katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao ili kufanya maamuzi ambayo yatakakuwa ya manufaa kwao.
Ni wito wake spika wa bunge la kaunti hii Catherine Mukenyang ambaye aidha amewataka wakazi kuwachaguzua viongozi kulingana na sera zao kwa taifa na kutokubali kushawishiwa kifedha na kufanya maamuzi ambayo watayajutia baadaye.
Wakati uo huo Mukenyang amewataka wakazi ambao hawajasajiliwa kuwa wapiga kura kutumia kipindi hiki ambacho mahakama iliagiza tume ya uchaguzi IEBC kuendeleza shughuli ya usajili wa wapiga kura wapya hadi tarehe 9 mjwezi huu kujitokeza na kusajiliwa.