WAKAZI POKOT MAGHARIBI WATAKIWA KUKUMBATIA TAMADUNI ZA KUNUFAISHA JAMII.


Katibu katika wizara ya michezo, utamaduni na toradhi za kitaifa Simon Kachapin ametoa wito kwa wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi kukumbatia na kudumisha mila na tamaduni zao na kutoziacha kudidimia.
Akizungumza wakati ambapo taifa limeadhimisha jana siku ya utamaduni kwa mara ya kwanza, tangu kutengwa kwa ajili ya kusherehekea utamaduni wa kiafrika na ambayo ilichukua nafasi ya sherehe za Moi day, kachapin ameelezea umuhimu wa wakenya kudumisha utamaduni wa kiafrika.
Hata hivyo kachapin ambaye pia alikuwa gavana wa kaunti hii ya pokot magharibi ametoa wito kwa wakazi wa kaunti hii kudumisha tamaduni zenye manufaa na zenye kuliwezesha taifa kusonga mbele na kujitenga na zile ambazo zimepitwa na wakati kama vile ukeketaji.