WAKAZI POKOT MAGHARIBI WATAKIWA KUJISAJILI KATIKA MAKUNDI ILI KUNUFAIKA NA ‘HUSTLER FUND’
Kama njia moja wepo ya kuinua makundi ya vijana na akina mama kaunti ya Pokot magharibi kupitia hazina ya serikali kuu ya serikali kuna haja ya wao kujiandikisha kwenye vikundi.
Mwenyekiti wa wahudumu wa boda boda katika soko la Tukum katika wadi ya Chepareria eneo bunge la Pokot kusini Philip Chepkoria amewahimiza wakazi hasa wahudumu wa boda boda kuhakikisha kwamba wanajiunga na makundi ili kupokea fedha hizo na kujiendeleza kimaisha, akisisi tiza kuwa riba watakayotakiwa kulipa baada ya kuchukua fedha hizo si ya juu.
“Nawahimiza watu wetu maeneo haya kuzingatia sana kujiunga na makundi ili wawe katika nafasi nzuri ya kupata fedha hizi. Pesa hizi hazina riba ya juu. Wakipata fedha hizi watajiendeleza katika maisha yao na watakaporejesha pesa za serikali watakuwa tayari wamepta faida.” Alisema Chepkoria.
Chepkoria pia aliwataka wenyeviti wa makundi mbali mbali ya wahudumu wa boda boda katika kaunti ya Pokot magharibi kuhakikisha kuwa wanawasajili wanachama wao katika makundi ili kupokea fedha hizo.
“Ombi langu ni kwa wenyeviti wa makundi ya boda boda kaunti hii kuhakikisha kwamba wanawasajili wanachama wao ili wanufaike na fedha hizi. Tutumie fursa hii ambayo serikali inanuia kuwainua kiuchumi wananchi wa hali ya chini kuhakikisha kwamba tunaimarika.” Alisema.