WAKAZI POKOT MAGHARIBI WATAKIWA KUENDELEA KUZINGATIA KANUNI ZA KUKABILI CORONA.


Kaunti ya Pokot magharibi imerekodi jumla visa 338 vya virusi vya corona tangu kuripotiwa nchini janga hilo mwezi machi mwaka jana.
Haya ni kwa mujibu wa mkurugenzi wa wizara ya afya katika kaunti hii ya pokot magharibi Dkt Nobert Abuya ambaye aidha amesema kati ya visa 3 hadi 7 hurekodiwa kila wiki kutokana vipimo 50 ambavyo huendeshwa katika kipindi hicho kutokana na mabadiliko ya sheria za kuendesha vipimo hivyo.
Aidha abuya ametoa wito kwa wakazi wa kaunti hii kuendelea kuzingatia kanuni za wizara ya afya katika kukabili msambao wa virusi vya corona ili kusalia salama ikizingatiwa taifa bado linakabiliwa na idadi kubwa ya maambukizi ya virusi hivyo.
Wakati uo huo Abuya amesema kufikia sasa ni wakazi alfu saba ambao wamepokea dozi ya kwanza ya chanjo dhidi ya virusi vya corona huku watu 2,500 wakiwa wamepokea dozi ya pili, akitoa wito kwa wakazi kuendelea kujitokeza kupokea chanjo hiyo ili kuwa na hakikisho la kinga dhidi ya covid 19.