WAKAZI POKOT MAGHARIBI WATAKIWA KUENDELEA KUTOA DAMU.
Wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi wametakiwa kuendelea kujitokeza kutoa damu ili kusaidia katika kukabili upungufu wa damu katika hospitali za Kapenguria, Kacheliba na Ortum.
Ni wito ambao umetolewa na msimamizi wa benki ya damu kaunti hii ya pokot magharibi Dkt. Jackson Ateleng ambaye amesema kuwa kuna hitaji kubwa la damu kaunti hii hasa kwa wagonjwa ambao wanafanyiwa upasuaji.
Akizungumza wakati wa shughuli ya kutoa damu iliyoandaliwa jana katika bustani ya Chelang’a mjini Makutano Ateleng amesema kuwa shughuli hiyo itaendelea juma hili hadi juma lijalo huku akiwataka wakazi kuendelea kujitokeza.