WAKAZI POKOT MAGHARIBI WATAKIWA KUENDELEA KUJITOKEZA KUSAJILIWA KUWA WAPIGA KURA.
Viongozi katika kaunti hii ya Pokot magharibi wameendelea kutoa wito kwa wakazi kujitokjeza kwa wingi kusajiliwa kuwa wapiga kura katika zoezi linaloendelezwa na tume ya uchaguzi na uratibu wa mipaka nchini IEBC la kuwasajili wapiga kura wapya.
Wa hivi punde kutoa wito huu ni mwakilishi wadi maalum Elijah Kasheusheu ambaye amesema kuwa ni kupitia hatua hiyo tu ambapo wakazi wa kaunti hii watapata fursa ya kuwachagua viongozi wanaowapendelea na kuwang’oa madarakani viongozi wasiowajibika kazini.
Wakati huo huo Kasheusheu ameitka serikali ya kaunti hii ya Pokot Magharibi kwa ushirikiano na serikali kuu kuhakikisha kuwa zinashughulikia halki ya baadhi ya barabara maeneo mbali mbali hasa mjini Makutano na viunga vyake anzosema zinatatiza shughuli za usafiri kwa wananchi.