WAKAZI POKOT MAGHARIBI WALALAMIKIA KUPANDA GHARAMA YA MAISHA.


Wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi wamelalamikia hali ngumu ya maisha ambayo wanakabiliana nayo.
Wakazizungumza mjini Makutano kaunti hii ya Pokot magharibi wakazi hao wamesema kuwa kwa sasa wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha kufuatia kupanda gharama nchini wakitaka serikali kuingilia kati na kuangazia hasa bei za bidhaa muhimu.
Kwa upande wao wafanyibiashara mjini Makutano wamelalamikia kupanda gharama ya kuagiza bidhaa hasa kufuatia kupanda bei za mafuta, hali ambayo wameihusisha na kusomwa bajeti majuzi ya kipindi cha mwaka wa kifedha 2021/2022.
Hata hivyo wakazi hao wamepongeza kupunguzwa karo katika shule za umma huku wakitoa wito kwa viongozi katika kaunti hii ya Pokot magharibi kufuatilia agizo hilo kuhakikisha kuwa wakuu wa shule katika kaunti hii wanapunguza karo hiyo.