WAKAZI POKOT MAGHARIBI WAHIMIZWA KUUNGA MKONO VYAMA VYA KISIASA VITAKAVYOWANUFAISHA.


Mwanasiasa yeyote ana uhuru na haki ya kuanzisha chama cha kisiasa katika kaunti hii ya Pokot magharibi.
Haya ni kwa mujibu wa mbunge wa Kapenguria Samwel Moroto ambaye hata hivyo amesema kuwa wakazi wa kaunti hii wanafaa kuwa makini na vyama wanavyounga mkono kuelekea uchaguzi mkuu akisisitiza haja ya wakazi kukumbatia vyama vitakavyowapa sauti katika maswala ya kitaifa.
Moroto ametumia fursa hiyo kukosoa mipangilio ya uongozi wa chama kipya kilichobuniwa katika kaunti hii na kuzinduliwa hivi majuzi cha KUP hatua anayodai inadhihirisha kukithiri maswala ya ukabila miongoni mwa viongozi.