WAKAZI POKOT MAGHARIBI WAHIMIZWA KUKUMBATIA VYUO VYA KIUFUNDI.
Na Benson Aswani
Wazazi kaunti hii ya Pokot magharibi wametakiwa kuhakikisha kuwa wanao ambao walifanya mtihani wa kidato cha nne na hawakufanikiwa kujiunga na vyuo vikuu wanajiunga na vyuo vya kiufundi ili kupata ujuzi wa kujiendeleza kimaisha.
Ni wito wake mkuu wa chuo cha kiufundi cha Kitalakapel kaunti hii ya Pokot magharibi John Kibowen ambaye amesema kuwa mafunzo yanayotolewa katika vyuo hivyo ni ya umuhimu mkubwa kwani yanampa mhusika fursa kubwa ya kujiajiri.
Aidha kibowen ametumia fursa hiyo kutoa mwito kwa serikali ya kaunti na wadau wengine kusaidia chuo hicho katika ujenzi wa miundo msingi ikiwemo madarasa zaidi pamoja na mabweni ili kutoa nafasi kwa wanafunzi wanotoka mbali kuhudhuria masomo bila tatizo.