WAKAZI POKOT MAGHARIBI WAHIMIZWA KUKUMBATIA MTAALA WA CBC.


Wito umetolewa kwa wazazi kukumbatia mtaala mpya wa elimu CBC unaotajwa kuwa wenye manufaa makubwa kwa wanafunzi.
Wakiongozwa na Albert Maindi mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya makutano Central na mwalimu wa mtaala wa CBC shule ya msingi ya Nasokol Carol Oloo, wadau katika sekta ya elimu kaunti hii ya Pokot magharibi wamesema kuwa licha ya pingamizi kutoka kwa baadhi ya wazazi, wanafunzi wengi wameweza kuukumbatia mtaala huo vyema.
Hata hivyo wamekiri kuwa mtaala huo ni ghali mno kwa wazazi ambao wana kipato cha chini kutokana na vifaa ambavyo vinahitajika ili kutumika na wanafunzi shuleni kutekeleza masomo.
Aidha wamelalamikia gharama ya juu ya mitihani ya wanafunzi kwa gredi ya tatu nne hadi tano ambayo inaendelea kwa sasa kutokana na changamoto iliyopo katika kuipata.