WAKAZI POKOT MAGHARIBI WAHAKIKISHIWA USALAMA MIPAKANI.
Wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi hasa katika mipaka ya kaunti hii na kaunti jirani ya Elgeyo marakwet ambako kumekuwa kukishuhudiwa utovu wa usalama wametakiwa kuendelea kudumisha amani msimu huu wa sherehe nyingi.
Akizungumza na kituo hiki kamanda wa polisi kaunti hii Jackson Tumwet aidha amewataka wazazi kuwa makini na kufuatilia mienendo ya wanao ili kuhakikisha kuwa hawajihusisha na vitendo vya utovu wa usalama msimu huu.
Tumwet ametoa wito pia kwa madereva kuwa makini na kufuata sheria za barabarani kwa kutojihusisha na vileo wakati wakiwa barabarani ili kuzuia visa vya ajali ambavyo huambatana mara nyingi na msimu huu.
Wakati uo huo Tumwet amewahakikishia wakazi kuwa usalama utaendelea kudumishwa kaunti hii hasa maeneo ya burudani pamoja na maeneo ya kuabudu kuhakikisha kuwa hakutaripotiwa visa vyovyote vya utovu wa usalama, doria anayosema itaendelezwa hadi wakati wanafunzi watakaporejea shuleni.