WAKAZI POKOT MAGHARIBI WACHANGAMKIA UJIO WA RAIS SAMIA NCHINI


Hisia mseto zimeendelea kuibuliwa nchini wananchi wakielezea matarajio yao kuhusu ziara ya rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan humu nchini.
Kulingana na wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi, ziara ya rais Samia humu nchini ni muhimu katika kuimarisha uhusiano wa kibiashara na kidiplomasia kufuatia mivutano ambao iUmekuwa Ukishuhudiwa katika siku za hivi karibuni baina ya mataifa haya mawili.
Aidha baadhi ya wakazi wamemtaka rais uhuru Kenyatta kutumia fursa ya ziara ya rais Samia kupata ushauri wa jinsi ya kukabili kukithiri visa vya wizi wa fedha za umma nchini.