WAKAZI POKOT KUSINI WALALAMIKIA HALI MBOVU YA BARABARA.
Kama njia moja ya kuimarisha uchumi wa wakazi wa wadi ya Chepareria Eneo bunge la Pokot Kusini kaunti ya Pokot magharibi, kuna haja ya Serikali kuu kukarabati nyingi za barabara hasa inayounganisha Chepareria na Ywalateke.
Wakazi wa eneo hilo walisema kwamba barabara za eneo hilo ni mbovu hali ambayo imeathiri pakubwa shughuli zao za kila siku.
Walisema kwamba imekuwa vigumu kwao kuafikia huduma muhimu ikiwemo za afya, kufuatia kupanda gharama ya usafiri kutokana na ubovu wa barabara za eneo hilo.
“Barabara za huku zimeharibika sana hasa kutoka Ywalateke kuelekea Chepareria. Tunapata wakati mgumu kusafiri kutafuta huduma muhimu kwa sababu bei ya usafiri imepanda sana. Tunaomba serikali ikarabati barabara hii ili pia tuafikie huduma muhimu.” Walisema wakazi.
Walisema kwamba itakuwa ni afueni kwao pamoja na wafanyibiashara ambao wanaendesha shughuli zao katika soko la Chepareria iwapo barabara hiyo itaweza kukarabatiwa.
“Iwapo barabara hii itatengenezwa tutapata afueni kwa sababu sasa gharama ya usafiri itapungua. Kwa sasa inatugharimu shilingi mia moja pahali ambapo tunafaa kulipia shilingi hamsini. Tuna imani na wizara ya Kipchumba Murkomen kwa sababu amezuru mara kadhaa eneo hili na kushuhudia jinsi hali ilivyo. Tunachoomba tu ni kuharakishwa mikakati ya kuikarabati.” Walisema.