WAKAZI NARAMAM WAONYWA DHIDI YA KUTOWAPELEKA WANAO SHULENI.


Wakazi wa eneo la Naramam kaunti hii ya Pokot magharibi wametakiwa kukumbatia elimu kwa wanao na kuwapeleka shuleni.
Ni wito wake naibu wa chifu eneo hilo Julius Korpira ambaye ameonya kuwa mzazi yeyote atakayepatikana na mwanawe nyumbani wakati anastahili kuwa shuleni atachukuliwa hatua kali kulingana na sheria.
Wakati uo huo Korpira amepongeza serikali ya kaunti kwa kufungua shule kadhaa za chekechea eneo hilo hali anayosema itapelekea kuimarika elimu, akizitaka kamati za shule hizo kuzisimamia vyema.