WAKAZI MIPAKANI PA POKOT MAGHARIBI NA ELGEYO MARAKWET WASHINIKIZA MIRADI YA MAENDELEO ILI KUKABILI TATIZO LA UTOVU WA USALAMA.


Uzinduzi wa miradi kama vile barabara utasaidia pakubwa katika kukabili utovu wa usalama ambao unashuhudiwa mara kwa mara mipakani pa kaunti hii ya Pokot magharibi na kaunti jiarani ya Elgeyo marakwet.
Haya ni kulingana na baadhi ya wenyeji wa maeneo hayo ambao wamesema ujenzi wa barabara kando na kurahisisha usafiri pia kutahakikisha kwamba maafisa wa usalama wanafika kwenye eneo litakovamiwa na majangili kwa wakati.
Aidha wenyeji hao wanasema kwamba maendeleo kwenye maeneo hayo pia yatawezesha biashara baina ya wakazi wa kaunti hizo mbili hivyo kupelekea wengi kuimarika kimaisha.