WAKAZI MAKUTANO WAACHWA VINYWA WAZI HUKU MKAZI MMOJA AKIFANYA HARUSI NA ‘MUNGU’


Wakazi mjini makutano kaunti hii ya Pokot magharibi waliachwa na mshangao baada ya mama mmoja kutoka eneo la Kalorema kujifanyia harusi mwenyewe katika bustani ya Chelang’a mjini Makutano kwa madai aliagizwa kufanya hivyo na Mwenyezi Mungu.
Elizabeth Nalem kutoka eneo la Kalorema kaunti hii ya Pokot magharibi anasema kuwa aliagizwa na Mwenyezi Mungu kufanya naye harusi na hata kuvishwa vazi la harusi kama ishara rasmi ya kuanza kumfanyia kazi.
Ni kisa ambacho mmewe ameelezea kushangazwa nacho huku akidai hali ya mkewe kubadili hadi kufikia kiwango cha kuchukua hatua hiyo imechochewa pakubwa na dhehebu ambalo amejiunga nalo katika siku za hivi karibuni.
Wakazi mjini Makutano ambao wameshuhudia kisa hicho katika bustani ya Chelang’a wameelezea kushangazwa nacho huku wakielezea kutilia shaka chanzo chake.