WAKAZI LOMUT POKOT MAGHARIBI WALALAMIKIA MAKALI YA NJAA.


Wakazi wa eneo la Lomut katika kaunti hii ya Pokot magharibi hasa walioyahama makwao kutokana na ukosefu wa usalama eneo la chesogon mpakani pa kaunti hii ya Pokot magharibi na kaunti jirani ya Elgeyo Marakwet wamelalamikia makali ya njaa eneo hilo wakitoa wito kwa viongozi kuingilia kati na kuwanusuru.
Wakiongozwa na Lomeri Lomeri Kaperur, wakazi hao wanadai kulazimika kutumia vyakula vinavyotajwa kuwa hatari kwa afya yao kwa kukosa namna.
Wamesema kuwa hali hiyo imepelekea ongezeko la utovu wa usalama ambapo baadhi ya wakazi sasa wanaendeleza wizi wa mifugo wakiuza ili kujikimu kimaisha.
Wametoa wito kwa viongozi wa eneo hilo wakiongozwa na mbunge wa Sigor Peter Lochakapong na serikali ya kuanti kwa jumla kushirikiana na kuhakikisha kuwa wakazi hao wanapata chakula haraka iwezekanavyo.