WAKAZI KERIO VALLEY WATAKIWA KUDUMISHA AMANI.


Jamii katika kaunti za bonde la kerio zimehimizwa kudumisha amani na kukoma visa vya wizi wa mifugo ili kutoa fursa ya kuendelezwa shughuli za maendeleo maeneo haya.
Akizungumza katika shule ya upili ya our lady of peace pser kaunti hii ya Pokot magharibi, mkuu wa elimu eneo la bonde la Ufa Jared Obiero amesema wanaoendekeza visa hivi wanafaa kufahamu enzi za uhalifu huo zilipita na sasa jamii inastahili kukumbatia amani.
Aidha Obiero ameelezea haja ya kujengwa shule zaidi maeneo yanayoshuhudiwa uvamizi huo akisema ndiyo njia ya pekee ya kuhakikisha amani inapatikana.
Wakati uo huo Obiero amewahikiza wakazi wa kaunti hii kukumbatia elimu ya wanao na kumpa fursa mtoto wa kike kutimiza ndoto zake kwa kujitenga na tamaduni ya ukeketaji na ndoa za mapema kwani pia zilipitwa na wakati.