WAKAZI KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI WATAKIWA KUZINGATIA UPANZI WA MITI.


Wito umetolewa kwa wakazi katika kaunti hii ya Pokot magharibi kuzingatia zaidi upanzi wa miti ili kutunza mazingira mbali na manufaa mengine mengi ambayo yantokana na miti.
Ni wito wake waziri wa barabara katika kaunti hii ya Pokot magharibi Joel Ng’asia akizungumza baada ya kushiriki zoezi la upanzi wa miti katika shule ya upili ya wasichana ya St. Elizas Kabichbich, ambaye aidha amewataka maafisa wa misitu kuhakikisha misitu inalindwa pamoja na kutoa elimu kwa wakazi kuhusu umuhimu wa kutunza misitu.
Ni kauli ambayo imetiliwa mkazo na chifu wa kata ya Lelan Daniel Ng’oriatudo ambaye aidha ametoa wito kwa serikali ya kaunti kununua miche zaidi ili kutoa fursa kwa wakazi kuendeleza zoezi hilo la upanzi wa miti.
Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Hellen Rono amesema wamepanda miche alfu 4 japo walilenga kupanda miche alfu10 huku akiwapongeza wadau wote ambao wameshiriki katika zoezi hilo na kusisitiza umuhimu wa uhifadhi wa misitu.