WAKAZI KATIKOMOR WALALAMIKIA KUTELEKEZWA KWA MASWALA YA MAENDELEO


Wakazi wa eneo la Katikomor kaunti hii ya Pokot magharibi wamelalamikia kutelekezwa eneo hilo kwa maswala ya maendeleo hasa miundo mbinu katika shule za eneo hilo.
Wakiongozwa na Cyrus Katikomor wakazi hao wamesema licha ya gavana wa John Lonyangapuo kudai kutekeleza miradi mbali mbali eneo hilo, hali ya baadhi ya shule ni mbovu huku wakitaka hatua kuchukuliwa kwa haraka ili kunusuru hali.
Aidha wakazi hao wamelalamikia hali mbaya ya barabara za eneo hilo wakidai pia kupoteza idadi kubwa ya mifugo baada ya kusombwa na maji ya mto Lomang’iro.