WAKAZI KATIKA BONDE LA KERIO WATAKIWA KUDUMISHA AMANI.


Wito umeyolewa kwa wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi, kaunti jirani ya Baringo pamoja na Turkana kuzingatia kuishi kwa amani na kukomesha uvamizi wa mara kwa mara unaochochewa na wizi wa mifugo.
Akizungumza katika mkutano wa amani eneo la Orolwo kaunti ya Turkana, naibu gavana kaunti ya Samburu Julius Leseto ameelezea haja ya wakazi wa kaunti hizi kushirikiana na magavana wao katika juhudi ambazo wanaendeleza kuhakikisha usalama unaafikiwa.
Loseto amesema kuwa eneo hili litaafikia maendeleo makubwa iwapo wakazi watashirikiana na kukomesha maswala ya wizi wa mifugo kwani kuna raslimali za kutosha kuafikia maendeleo hitajika.