WAKAZI BARINGO WASHAURIWA KUTILIA MAANANI MASHARTI YA KUKABILI CORONA.


Wakazi kaunti ya Baringo wameshauriwa kuendelea kufuata masharti ya wizara ya afya ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona kwani ni jukumu la mtu binafsi kujilinda dhidi ya ugonjwa wa Covid 19.
Akiongea katika eneo la Kapkiamo mwaniaji wa wadhifa wa uwakilishi akina mama kupitia chama cha UDA Rebecca Lomong amesema pana haja ya kila mmoja kufuata masharti yaliyowekwa kama vile kuvalia maski, ikizingatiwa aina mpya ya corona ya omicron inaenea kwa kasi.
Lomong’ aidha amesisitiza haja ya kila mkazi wa Baringo kupokea chanjo dhidi ya ugonjwa wa Covid 19 akisema kwamba wale watakaochanjwa hawataathirika zaidi iwapo watapatwa na virusi vya Corona.
Kando na hayo Lomong’ amewahimiza wazazi kuwa karibu na wanao na kufuatilia mienendo yao kabla ya shule kufunguliwa wiki ijayo ili kuhakikisha kwamba hawapotoki kimaadili.